Kanisa Katoliki la Kimelkiti
From Wikipedia, the free encyclopedia
Kanisa Katoliki la Kimelkiti (kwa Kiarabu: كنيسة الروم الملكيين الكاثوليك, Kanīsat ar-Rūm al-Malakiyyīn al-Kāṯūlīk) ni mojawapo kati ya madhehebu ya Kanisa Katoliki yanayoongozwa na Patriarki wake akisaidiwa na sinodi yake na akiwa na ushirika kamili na Papa wa Roma tangu mwaka 1729.
Maelezo zaidi Imani, Muundo ...
Funga
Makao makuu yako Damasko, Siria, lakini Patriarki anatumia jina la Antiokia na mashariki yote, Aleksandria na Yerusalemu.
Kwa sasa (tangu tarehe 21 Juni 2017) Patriarki ni Youssef Absi, S.M.S.P., anayetokea Damasko.
Kwa asili waamini wake wengi (milioni 1.6) wanazungumza Kiarabu, lugha rasmi ya Kanisa hilo, ingawa hasa siku hizi wana mchanganyiko mkubwa wa damu.