Historia ya Utawa
From Wikipedia, the free encyclopedia
Hatuwezi kuelewa utawa tukidhani ni kitu kimoja: jina hilo linajumlisha maisha tofautitofauti.
Maelezo zaidi Imani, Muundo ...
Funga
Katika makala hii tunataka kufuata historia ya maisha haya katika Ukristo kama kitabu bora kilichoandikwa na Mungu siku kwa siku kadiri ya mpango wake wa hekima kwa ujenzi wa Kanisa lake takatifu kwa karama za kumshuhudia Yesu katika sifa na kazi zake mbalimbali.
Kuna hatua kuu nne zilipozaliwa aina mpya za utawa (hasa magharibi) bila ya kufuta zile zilizotangulia:
- 1. Kuanzia karne III hadi XII ulitawala umonaki ukifuatwa na ukanoni.
- 2. Kuanzia karne XIII yalistawi hasa mashirika ya ombaomba.
- 3. Kuanzia karne XVI yalitokea mashirika mengi ya kikleri, yasiyo na nadhiri na ya kutolea huduma maalumu.
- 4. Hatimaye karne XX yalikubaliwa mashirika ya kilimwengu na kuanzishwa jumuia mpya.