Etna
From Wikipedia, the free encyclopedia
Etna (kutoka Kilatini: Aetna; kwa Kiitalia pia Mongibello; kwa Kisisili Mungibeddu au â Muntagna) ni volkeno hai wa Sicilia mashariki (Italia visiwani) kati ya miji ya Catania na Messina. Ndiyo ndefu kuliko zote za Ulaya[1]: kwa sasa imefikia mita 3357 juu ya usawa wa bahari.[2]
Kwa maana nyingine, tazama Etna (maana).
Etna inaenea katika kilometa mraba 1190 ukiwa na duara ya km 140 miguuni pake. [3]
Etna inakadiriwa kuwa na miaka 350,000 - 500,000 na ni kati ya volkeno hai zaidi duniani, kwa kuwa haitulii karibu kamwe, lakini kwa namna yake si hatari. Lava yake inageuka baada ya miaka kadhaa kuwa nzuri sana kwa kilimo.
Mnamo Juni 2013 iliingizwa na UNESCO katika orodha ya urithi wa dunia.[4]