Kisisili
From Wikipedia, the free encyclopedia
Kisisili (kwa lugha hiyo: Sicilianu) ni mojawapo kati ya Lugha za Kirumi, ingawa asilimia 20 za maneno yake yana asili ya Kigiriki na Kiarabu.
Ndiyo ya kwanza kuwa na fasihi katika ya lugha za Italia.
Hadi leo inatumiwa na watu milioni 5 hivi, hasa katika sehemu kubwa kabisa ya kisiwa cha Sicilia, lakini pia Italia Kusini na kokote walikohamia wenyeji wa sehemu hizo.