Siku tatu kuu za Pasaka
From Wikipedia, the free encyclopedia
Siku tatu kuu za Pasaka ndizo kiini cha mwaka wa Kanisa.
Zimekusudiwa kumuadhimisha Yesu mteswa, mzikwa na mfufuka, yaani:
- siku ya kwanza (Alhamisi kuu jioni hadi Ijumaa kuu jioni) inaadhimisha mateso yake kuanzia karamu ya mwisho hadi kifo chake juu ya msalaba;
- siku ya pili (Ijumaa kuu jioni hadi Jumamosi kuu jioni) inaadhimisha maiti yake kubaki kaburini na roho yake kushukia kuzimu;
- siku ya tatu (kuanzia Jumamosi kuu jioni hadi Jumapili ya Pasaka jioni) inaadhimisha ufufuko wake mtukufu.
Siku hizo tatu ni kama bawaba kati ya Kwaresima na kipindi cha Pasaka. Ingawa tarehe zinabadilika kila mwaka, zinaangukia daima kati ya Machi mwishoni na Aprili mwishoni.