Sherehe kuu
From Wikipedia, the free encyclopedia
Sherehe kuu 12 (kwa Kigiriki: Δωδεκάορτον, Dodekaorton) za Makanisa ya Kiorthodoksi, tukiacha Pasaka iliyo sikukuu ya sikukuu zote, zinawaadhimisha Yesu Kristo (8) pamoja na Bikira Maria (4).[1]
Ni hizi zifuatazo:
- 21 Septemba [O.S. 8 Septemba], Kuzaliwa kwa Mama wa Mungu
- 27 Septemba [O.S. 14 Septemba], Kutukuka kwa Msalaba
- 4 Desemba [O.S. 21 Novemba], Mama wa Mungu kutolewa hekaluni
- 7 Januari [O.S. 25 Desemba], Kuzaliwa kwa Kristo/Krismasi
- 19 Januari [O.S. 6 Januari], Ubatizo wa Kristo — Theofania, inayoitwa pia Epifania
- 15 Februari [O.S. 2 Februari], Yesu kutolewa hekaluni
- 7 Aprili [O.S. 25 Machi], Kupashwa Habari Maria
- Jumapili kabla ya Pasaka — Kuingia Yerusalemu Jumapili ya Matawi au ya Mitende au ya Maua
- Siku arubaini baada ya Pasaka — Yesu Kristo Kupaa Mbinguni
- Siku hamsini baada ya Pasaka — Pentekoste
- 19 Agosti [O.S. 6 Agosti], Yesu Kugeuka Sura
- 28 Agosti [O.S. 15 Agosti], Kulala kwa Mama wa Mungu
Mbali ya hizo, Waorthodoksi wana sherehe nyingine tano zinaazohesabiwa kuwa kuu: Tohara ya Kristo 14 January [O.S. 1 January], Kuzaliwa kwa Yohane Mbatizaji 7 Julai [O.S. 24 Juni], Watakatifu Petro na Paulo 12 July [O.S. 29 June], Kukatwa Kichwa kwa Yohane Mbatizaji 11 Septemba [O.S. 29 Agosti], na Ulinzi wa Mama wa Mungu 14 Oktoba [O.S. 1 Oktoba].[2]