Kinubi
From Wikipedia, the free encyclopedia
Vinubi ni ndege wakubwa kiasi wa jenasi mbalimbali katika familia Corvidae. Kinubi mkia-kahawia huitwa kinubi kwa ufupi pia. Ndege hawa hawana wote mhenga mmoja. Mkia wao ni mrefu kuliko ule wa kunguru. Spishi nyingi ni nyeusi au nyeusi na nyeupe; nyingine zina rangi ya buluu, ya majani au ya kahawa. Wanatokea Amerika ya Kaskazi, Ulaya, Afrika na Asia. Hula nusra kila kitu: wanyama na ndege wadogo, wadudu, mizoga, matunda, nafaka n.k. Hulijenga tago lao kwa vijiti mtini. Jike huyataga mayai 5-10.
Maelezo zaidi Uainishaji wa kisayansi ...
Kinubi | ||||||||||||||||
---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
Kinubi mkia-kahawia | ||||||||||||||||
Uainishaji wa kisayansi | ||||||||||||||||
| ||||||||||||||||
Funga