Shomoro ni ndege wadogo wa jenasi Passer katika familia ya Passeridae ambao wana rangi ya nyeusi, nyeupe, majivu na kahawia. Ndege hawa huitwa korobindo pia, lakini jina hili litumike afadhali kwa kuita ndege wa jenasi Petronia. Shomoro wenye kichwa kijivu huitwa jurawa. Ndege hawa wana domo fupi na nene lifaalo kula mbegu, lakini hula wadudu wadogo pia hasa wanapokuwa vifaranga. Kwa asili shomoro wanatokea Ulaya, Afrika na Asia, lakini watu wamewaletea Australia na Marekani.
Maelezo zaidi Uainishaji wa kisayansi, Ngazi za chini ...
Shomoro |
Shomoro mwekundu |
Uainishaji wa kisayansi |
Himaya: |
Animalia (Wanyama)
|
Faila: |
Chordata (Wanyama wenye ugwe wa neva mgongoni)
|
Ngeli: |
Aves (Ndege)
|
Oda: |
Passeriformes (Ndege kama shomoro)
|
Familia ya juu: |
Passeroidea
|
Familia: |
Passeridae (Ndege walio na mnasaba na shomoro)
|
Jenasi: |
Passer (Shomoro na jurawa) Brisson, 1760 |
|
Ngazi za chini |
Spishi 28:
- P. ammodendri (Gould, 1872)
- P. castanopterus (Blyth, 1855)
- P. cinnamomeus (Gould, 1836)
- P. cordofanicus (Heuglin, 1871)
- P. diffusus (A. Smith, 1836)
- P. domesticus (Linnaeus, 1758)
- P. eminibey (Hartlaub, 1880)
- P. euchlorus (Bonaparte, 1850)
- P. flaveolus (Blyth, 1845)
- P. gongonensis (Oustalet, 1890)
- P. griseus (Vieillot, 1817)
- P. hemileucus Ogilvie-Grant & H.O.Forbes, 1899
- P. hispaniolensis (Temminck, 1820)
- P. iagoensis (Gould, 1837)
- P. insularis (Sclater & Hartlaub, 1881)
- P. italiae (Vieillot, 1817)
- P. luteus (Lichtenstein, 1823)
- P. melanurus (Statius Müller, 1776)
- P. moabiticus (Tristram, 1864)
- P. motitensis (A.Smith, 1848)
- P. pyrrhonotus (Blyth, 1845)
- P. rufocinctus (Fischer & Reichenow, 1884)
- P. shelleyi Sharpe, 1891
- P. simplex (Lichtenstein, 1823)
- P. suahelicus (Reichenow, 1904)
- P. swainsonii (Rüppell, 1840)
- P. zarudnyi Pleske, 1896
|
Funga