Petro Favre
From Wikipedia, the free encyclopedia
Petro Favre (kwa Kifaransa Pierre Favre au Pierre Lefevre; Villaret, Savoie, leo nchini Ufaransa, 13 Aprili 1506 - Roma, Italia, 1 Agosti 1546) alikuwa padri wa kwanza na mwanzilishi mwenza wa Shirika la Yesu pamoja na Ignas wa Loyola na Fransisko Saveri.
Kwa utiifu alitimiza majukumu mazito katika sehemu mbalimbali za Ulaya, akafariki akiwa anajiandaa kwenda Italia Kaskazini kushiriki mtaguso mkuu wa Trento[1].
Alitangazwa na Papa Pius IX kuwa mwenye heri tarehe 5 Septemba 1872, halafu Papa Fransisko alimtangaza mtakatifu tarehe 17 Desemba 2013[2].