Fransisko Saveri
From Wikipedia, the free encyclopedia
Fransisko Saveri ni jina la kawaida la Francisco de Jasso y Azpilicueta (Javier, Navarra, leo nchini Hispania, 7 Aprili 1506 - kisiwa cha Shangchuan, China, 3 Desemba 1552) alikuwa padri wa Shirika la Yesu, ambalo alichangia kulianzisha pamoja na Ignas wa Loyola.
Baadaye alitangaza Injili katika nchi nyingi za Ulaya, Afrika na Asia hata akawa kati ya wamisionari maarufu zaidi ya historia ya Kanisa.
Alitangazwa na Papa Paulo V kuwa mwenye heri tarehe 25 Oktoba 1619, halafu Papa Gregori XV akamtangaza mtakatifu tarehe 12 Machi 1622.
Anaheshimiwa na Waanglikana na Walutheri pia.