Malakia wa Armagh
From Wikipedia, the free encyclopedia
Malakia wa Armagh (jina asili la Kieire: Máel Máedóc Ua Morgair;; Armagh, Ireland, 1094 - Clairvaux, Ufaransa, 2 Novemba 1148) alikuwa mkaapweke, padri, abati, halafu askofu (1124) wa Cannoret, tena wa Down na Connor, Ireland, alipoanzisha jumuia ya Wakanoni[1].
Alifariki katika monasteri ya Bernardo wa Clairvaux, aliyeandika maisha yake[2] .
Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki kama mtakatifu.