Dimitri wa Thesalonike
From Wikipedia, the free encyclopedia
Dimitri wa Thesalonike (kwa Kigiriki Άγιος Δημήτριος της Θεσσαλονίκης; alifariki 306 hivi) alikuwa Mkristo wa mkoa wa Panonia (leo nchini Kroatia) ambaye alifia dini yake katika dhuluma ya Kaisari Dioklesyano.
Kwa sababu hiyo tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki, Waorthodoksi na Waorthodoksi wa Mashariki kama mtakatifu.
Sikukuu yake huadhimishwa katika tarehe mbalimbali; kwa Wakatoliki ni tarehe 9 Aprili[1].