Bikira Maria wa Mlima Karmeli
From Wikipedia, the free encyclopedia
Bikira Maria wa Mlima Karmeli ni jina linalopewa Bikira Maria kama msimamizi wa Wakarmeli. Wa kwanza wao walikuwa wakaapweke walioishi mwishoni mwa karne ya 12 na mwanzoni mwa karne ya 13 katika Nchi Takatifu juu ya Mlima Karmeli, ambapo zamani Nabii Eliya alirudisha Waisraeli kumuabudu Mungu aliye hai.
Katikati ya makazi yao walijenga kikanisa kwa heshima ya Bikira Maria, msimamizi wao.
Tangu karne ya 15 watu wamemheshimu kwa jina hilo hasa kwa kuvaa skapulari ya kahawia inayosemekana Maria alimpa Mkarmeli Simoni Stock (1165-1265).
Kumbukumbu katika liturujia inafanyika tarehe 16 Julai.[1][2][3][2]