Arseni Mkuu
From Wikipedia, the free encyclopedia
Arseni Mkuu, au Arseni shemasi au Arseni wa Scetis au Arseni Mrumi (Roma, 350/354 - Troe, Misri 445) alikuwa msomi na tajiri wa Roma ambaye, baada ya kulea watoto wa kaisari Theodosius I kwa miaka 11, akiwa shemasi, alihamia jangwani huko Misri ili aishi kama mkaapweke kwa miaka 55.
Ni kati ya mababu wa jangwani walioacha athari kubwa zaidi katika maisha ya Kiroho ndani ya Kanisa[1], ndiyo sababu aliitwa "mkuu".
Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki, Waorthodoksi na Waorthodoksi wa Mashariki kama mtakatifu.
Sikukuu yake huadhimishwa kwa kawaida tarehe 8 Mei[2], isipokuwa na Wakhufi[3][4].