Amato Ronconi
From Wikipedia, the free encyclopedia
Amato Ronconi (Saludecio, Rimini, Italia, 1225 hivi - Saludecio, 8 Mei 1292 hivi) alikuwa Mkristo maarufu kwa kuishi miaka mingi kwa toba na hija. Alijenga makanisa na vituo vya kuhudhumia kwa ukarimu mkubwa wasafiri na maskini, ambao aliwagawia mali yake yote[1].
Kwa sababu hizo, wengine wanasema alikuwa Mfransisko wa Utawa wa Tatu[2].
Tangu kale anaheshimiwa kama mtakatifu. Hiyo ilithibitishwa kwanza na Papa Pius VI tarehe 17 Aprili 1776, halafu na Papa Fransisko tarehe 23 Novemba 2014[3].