Yohane wa Sahagun
From Wikipedia, the free encyclopedia
Yohane wa Sahagun, O.E.S.A. (Sahagun, Leon, Hispania, 24 Juni 1419 - Madrid, Hispania, 11 Juni 1479) alikuwa padri mwanajimbo aliyejiunga na shirika la Waaugustino akapata umaarufu kwa mahubiri yake na kwa maisha ya kiroho yaliyomwezesha kurudisha amani kati ya wananchi waliogawanyika makundimakundi kwa chuki[1][2].
Papa Klementi VIII alimtangaza mwenye heri mwaka 1601, halafu Papa Aleksanda VIII akamtangaza mtakatifu tarehe 16 Oktoba 1690.
Sikukuu yake inaadhimishwa kila mwaka tarehe ya kifo chake[3].