Vita vya tatu vya Kiyahudi
From Wikipedia, the free encyclopedia
Vita vya tatu vya Kiyahudi dhidi ya Warumi (132ā136 BK) vilifanyika hasa katika Yudea, sehemu ya Dola la Roma.
Vilifuata vile vya kwanza (66-73) vilivyotokea katika Yudea na vya pili (115ā117), hasa nje ya Palestina (Libya, Misri, Kupro na Mesopotamia).
Pamoja na ushujaa wa Wayahudi waliopigania uhuru wa nchi yao chini ya Simoni Bar Kokhba, hatimaye Warumi walipata ushindi, waliangamiza Wayahudi wengi, walifuta mamlaka yao ya ndani na kuwafukuza moja kwa moja kutoka Yerusalemu iliyojengwa upya kama mji wa Kiroma uliotwa "Aelia Capitolina". Wayahudi waliruhusiwa kuutembelea lakini waliweza kurudi tu baada ya uvamizi wa Kiislamu mnamo mwaka 638.