Vita vya kwanza vya Kiyahudi
From Wikipedia, the free encyclopedia
Vita vya kwanza vya Kiyahudi dhidi ya Warumi (66–73 BK) vilifanyika hasa katika Yudea, sehemu ya Dola la Roma.
Vilifuatwa na vya pili (115–117), hasa nje ya Palestina (Libya, Misri, Kupro na Mesopotamia), na vya tatu (132–136), tena katika Yudea.
Pamoja na ushujaa wa Wayahudi waliopigania uhuru wa nchi yao, hatimaye Warumi waliteka na kuangamiza Yerusalemu na hekalu lake (70).
Habari hizo zilisimuliwa hasa na mwanahistoria Yosefu Flavius.