Vikta na Korona
From Wikipedia, the free encyclopedia
Vikta na Korona (walifariki Syria, karne ya 2 hivi) walikuwa Wakristo walioteswa na hatimaye kuuawa katika dhuluma ya Dola la Roma [1].
Vikta alikuwa askari ambaye, wakati wa kuteswa kwa ajili ya imani yake, alitiwa moyo na Korona, msichana wa miaka 16 aliyekwishaolewa na askari mwingine[2][3][4].
Hatimaye Vikta alikatwa kichwa, Korona aliraruliwa vipandevipande akiwa hai.
Tangu kale Kanisa linawaheshimu kama watakatifu wafiadini.