Ubepari
From Wikipedia, the free encyclopedia
Ubepari ni mfumo wa uchumi ambamo biashara, viwanda na vitegauchumi vingine vinatawaliwa na watu binafsi kwa kiasi kikubwa na kwa lengo la kupata faida. Nafasi ya serikali ni ndogo. Vilevile lengo la kuhudumia jamii katika mahitaji yake haliongozi mipango.[1][2]
Kati ya sifa za ubepari kuna ulimbikizaji wa mtaji, ushindani katika soko huria na kazi zinazolipwa mshahara.[3]
Katika mfumo huo, pande zinazokabiliana zinapanga zenyewe bei kwa makubaliano, bila kuingiliwa na mamlaka yoyote ya nje.[4]
Ubepari una viwango tofauti vya uhuru huo, kadiri ya nchi:[5]Kiingereza kinaainisha laissez-faire capitalism, welfare capitalism, crony capitalism na state capitalism.[6]