Sifaka (kutoka Kimalagasi: sifaka) ni spishi za lemuri wa jenasi Propithecus katika familia Indriidae. Kama lemuri wote wanatokea Madagaska tu. Jina lao linafanana na sauti yao: “shi-fak”. Manyoya yao ni marefu na laini kama hariri. Rangi yao ni nyeupe, kahawia au nyeusi au muunganisho wa rangi hizi. Uso wao ni mweusi. Mwili wa wanyama hawa una urefu wa sm 40-55 na uzito wao ni kg 3-6. Urefu wa mkia ni sawa na mwili. Hula majani, maua na matunda.
Maelezo zaidi Uainishaji wa kisayansi, Ngazi za chini ...
Sifaka |
Sifaka taji |
Uainishaji wa kisayansi |
Domeni: |
Eukaryota (Viumbe walio na seli zenye kiini)
|
Himaya: |
Animalia (Wanyama)
|
Faila: |
Chordata (Wanyama wenye ugwe wa neva mgongoni)
|
Ngeli: |
Mamalia (Wanyama wenye viwele wanaonyonyesha wadogo wao)
|
Oda: |
Primates (Wanyama wanaofanana kiasi na binadamu)
|
Nusuoda: |
Strepsirrhini (Wanyama wanaofanana zaidi na lemuri)
|
Oda ya chini: |
Lemuriformes (Wanyama kama kima)
|
Familia ya juu: |
Lemuroidea (Lemuri)
|
Familia: |
Indriidae (Lemuri walio na mnasaba na indri)
|
Jenasi: |
Propithecus Bennett, 1832 |
|
Ngazi za chini |
Spishi
- P. candidus A. Grandidier, 1871
- P. coquereli (A. Grandidier, 1867)
- P. coronatus Milne-Edwards, 1871)
- P. deckenii A. Grandidier, 1867
- P. diadema Bennett, 1832
- P. edwardsi A. Grandidier, 1871
- P. perrieri Lavauden, 1931
- P. tattersalli Simons, 1988
- P. verreauxi A. Grandidier, 1867
|
Funga