Roderiki na Solomoni
From Wikipedia, the free encyclopedia
Roderiki na Solomoni (walifariki Cordoba, Hispania, 13 Machi 857) walikuwa watu wa Hispania waliouawa na Waislamu waliotawala nchi hiyo kwa sababu ya imani yao ya Kikristo.
Padri Roderiki alipokataa kusadiki kwamba Muhamadi alikuwa kweli nabii kutoka kwa Mwenyezi Mungu, alitupwa gerezani alipokutana na Solomoni, ambaye alikuwa amewahi kusilimu kwa muda fulani; hatimaye walishinda jaribu lao kwa kukatwa kichwa.[1] na mwingine mwenzake gerezani[2]
Tangu kale wanaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama watakatifu wafiadini.