Ramon wa Fitero
From Wikipedia, the free encyclopedia
Ramon wa Fitero (pia: Raimundo, Raymond; karne ya 12 - 1163) alikuwa padri kanoni, halafu mmonaki na hatimaye abati wa monasteri ya mji huo, mwanzilishi wa shirika la kijeshi la Calatrava na mkombozi mkubwa wa Wakristo nchini Hispania[1].
Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki kama mtakatifu. Heshima hiyo ilithibitishwa na Papa Klementi XI mwaka 1719.
Sikukuu huadhimishwa tarehe 1 Februari[2].