Qasim Amin
mwandishi, hakimu na mrekebishaji wa kijamii / From Wikipedia, the free encyclopedia
Qasim Amin (hutamkwa [ˈʔæːsem ʔæˈmiːn], Kiarabu cha Misri: قاسم أمين; Aleksandria, 1 Desemba 1863 [1] - Kairo, 22 Aprili 1908) alikuwa mwanasheria wa Misri, Mwislamu wa kisasa[2] na mmoja wa waanzilishi wa harakati za kitaifa za Misri na Chuo Kikuu cha Kairo.
Qasim Amin kihistoria anaonekana kama ni mwanaharakati wa kwanza kutetea haki za wanawake kutokea Uarabuni ingawa alijiunga na mjadala wa utetezi wa wanawake unaorudisha nyuma maendeleo[3]