Petro I wa Aleksandria
From Wikipedia, the free encyclopedia
Petro I wa Aleksandria alikuwa Papa wa 17 wa Kanisa la Kikopti na alifia dini ya Ukristo tarehe 25 Novemba 311 chini ya kaisari Dioklesyano.
Pamoja naye waliuawa maaskofu Esiki, Pakomi na Theodori, mapadri Fausto, Dio na Amoni na wengine wengi.
Tangu kale anaheshimiwa na Waorthodoksi wa Mashariki, Waorthodoksi na Wakatoliki kama mtakatifu.[1]