Marselo wa Tanja
From Wikipedia, the free encyclopedia
Marselo wa Tanja (au Marselo akida) alikuwa askari Mkristo huko Tanja (leo nchini Moroko) aliyefia dini yake kwa kukatwa kichwa katika dhuluma ya kaisari Diocletian mwanzoni mwa karne ya 4.
Tarehe inayotajwa na mapokeo ni 3 Desemba 298[1].
Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu mfiadini.