Maria Maajabu wa Yesu
From Wikipedia, the free encyclopedia
Maria Maajabu wa Yesu, O.C.D. (Madrid, Hispania, 4 Novemba 1891 - La Aldehuela, 11 Desemba 1974) alikuwa mmonaki bikira anayeheshimiwa na Kanisa Katoliki kama mtakatifu bikira.
Papa Yohane Paulo II alimtangaza mwenye heri tarehe 10 Mei 1998 akamtangaza mtakatifu tarehe 4 Mei 2003.
Sikukuu yake inaadhimishwa kila mwaka tarehe 11 Desemba[1].