Makanisa ya Bikira Maria
From Wikipedia, the free encyclopedia
Makanisa ya Bikira Maria ni maabadi ya Kikristo ambapo mama wa Yesu anaheshimiwa kwa namna ya pekee, kwa kuwa ama aliishi huko, ama alitokea ama alifanya muujiza, ama waumini wenyewe walijisikia hamu ya kuonyesha shukrani yao kwake.
Makanisa ya namna hiyo yalijengwa tangu karne za kwanza za historia ya Ukristo, hasa baada ya Hati ya Milano iliyowapa wananchi uhuru wa dini katika Dola la Roma[1][2][3], na siku hizi zinapatikana katika mabara yote, hata Antaktiki.
Mara nyingi ni patakatifu palipo lengo la hija hasa ya Wakristo wa madhehebu mbalimbali.
Kubwa kuliko yote ni Basilika la Bikira Maria Aparecida, Brazil, ambalo limezidiwa tu na Basilika la Mt. Petro huko Roma-Vatikano.