Lemuri-panya (kutoka Kiingereza: mouse lemur) ni spishi za lemuri wa jenasi Microcebus katika familia Cheirogaleidae. Kama lemuri wote wanatokea Madagaska tu. Urefu wa jumla wa kichwa, mwili na mkia ya lemuri-panya ni chini ya sm 27, kwa hivyo wao ni wadogo kuliko primates wote. Hukiakia usiku na hula arthropodi, vertebrati wadogo, vinyaa vya wadudu, ambo la miti, matunda, maua na mbochi, na majani na matumba pia kufuatana na majira.
Maelezo zaidi Uainishaji wa kisayansi, Ngazi za chini ...
Lemuri-panya |
Lemuri-panya kijivu |
Uainishaji wa kisayansi |
Domeni: |
Eukaryota (Viumbe walio na seli zenye kiini)
|
Himaya: |
Animalia (Wanyama)
|
Faila: |
Chordata (Wanyama wenye ugwe wa neva mgongoni)
|
Ngeli: |
Mamalia (Wanyama wenye viwele wanaonyonyesha wadogo wao)
|
Oda: |
Primates (Wanyama wanaofanana kiasi na binadamu)
|
Nusuoda: |
Strepsirrhini (Wanyama wanaofanana zaidi na lemuri)
|
Oda ya chini: |
Lemuriformes (Wanyama kama kima)
|
Familia ya juu: |
Lemuroidea (Lemuri)
|
Familia: |
Cheirogaleidae (Lemuri walio na mnasaba na lemuri kibete)
|
Jenasi: |
Microcebus E. Geoffroy, 1828 |
|
Ngazi za chini |
Spishi 21:
- M. arnholdi E. Lewis Jr. et al., 2008
- M. berthae Rasoloarison et al., 2000
- M. bongolavensis Olivieri et al., 2007)
- M. boraha Hotaling et al., 2016)
- M. danfossi Olivieri et al., 2007
- M. ganzhorni Hotaling et al., 2016
- M. gerpi Radespiel et al., 2012
- M. griseorufus Kollman, 1910
- M. jollyae Louis et al., 2006
- M. lehilahytsara Roos & Kappeler, 2005
- M. macarthurii Radespiel et al., 2008
- M. mamiratra Andriantompohavana et al., 2006
- M. manitatra Hotaling et al., 2016
- M. margotmarshae Andriantompohavana et al., 2006
- M. marohita Rasoloarison et al., 2013
- M. mittermeieri Louis et al., 2006
- M. murinus (J.F. Miller, 1777)
- M. myoxinus Peters, 1852
- M. ravelobensis Zimmermann et al., 1998
- M. rufus E. Geoffroy, 1834
- M. sambiranensis Rasoloarison et al., 2000
- M. simmonsi Louis et al., 2006
- M. tanosi Rasoloarison et al., 2013
- M. tavaratra Rasoloarison et al., 2000
|
Funga