Lazaro Devasahayam Pillai
From Wikipedia, the free encyclopedia
Lazaro Devasahayam Pillai (23 Aprili 1712 - 14 Januari 1752) alikuwa Mkristo wa India aliyefia dini yake nchini mwake kwa kukataa kurudia dini ya Uhindu[1].
Papa Benedikto XVI alimtangaza mwenye heri tarehe 2 Desemba 2012 halafu Papa Fransisko akamtangaza mtakatifu tarehe 15 Mei 2022.
Sikukuu yake huadhimishwa kila mwaka tarehe 14 Januari[2].