Kongo (mto)
Mto wa Kongo (kati ya miaka 1971 na 1997 uliitwa zaidi "Zaire") ni mto mkubwa wa Afrika ya kati. Ni mto mrefu wa pili katika Afrika baada ya Nile. Pia ni mto wenye kina kirefu zaidi duniani. / From Wikipedia, the free encyclopedia
Mto wa Kongo (kati ya miaka 1971 na 1997 uliitwa zaidi "Zaire") ni mto mkubwa wa Afrika ya kati. Ni mto mrefu wa pili katika Afrika baada ya Nile. Pia ni mto wenye kina kirefu zaidi duniani.
Ukweli wa haraka Mto wa Kongo ...
Chanzo | Katika milima ya Mitumba takr. 100 km magharibi ya Lumbumbashi (Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo) |
Mdomo | Atlantiki |
Nchi | Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Jamhuri ya Kongo |
Urefu | 4,700 km |
Kimo cha chanzo | 1,400 m |
Mkondo | 42,000 m³/s |
Eneo la beseni | 3,730,000 km² |
Idadi ya watu wanaokalia beseni | milioni 56 |
Miji mikubwa kando lake | Kisangani, Mbandaka, Kinshasa, Brazzaville, Matadi |
Funga
Beseni la Kongo pamoja na matawimto yake ni eneo kubwa la pili duniani la msitu wa mvua. Kwa kiasi cha mshuko wa maji mdomoni ni mto mkubwa wa pili duniani baada ya Amazonas (Amerika ya Kusini).[1]
Urefu wake ni kilomita 4,700 ukipimwa kuanzia chanzo cha tawimto la mbali zaidi ambalo ni mto Chambeshi wenye chanzo nchini Zambia. Mara nyingi urefu hutajwa kuanzia chanzo cha Lualaba halafu ni kilomita 4,374.