Klara wa Asizi
From Wikipedia, the free encyclopedia
Klara wa Asizi (Assisi, Umbria, Italia 16 Julai 1193 - Assisi, 11 Agosti 1253) ni mwanamke wa kwanza kujiunga na tapo la toba la Fransisko wa Asizi tena ni mwanamke wa kwanza kutunga kanuni ya kitawa katika historia ya Kanisa.
Huyo bikira, anayehesabika kuwa mwanzilishi mwenza wa Mabibi Fukara wa Utawa wa Ndugu Wadogo, alipenda kujiita mche mdogo wa Fransisko, akimfuata kiroho kwa kuishi katika mji wao toba kali iliyojaa matendo ya upendo na ibada. Akipenda kwa namna ya pekee ufukara wa hiari, hakukubali kamwe kuachanishwa nao, hata alipopatwa na hali ya kuhitaji na kuugua sana[1].
Anaheshimiwa na Kanisa Katoliki kama mtakatifu na msimamizi wa televisheni.