Kaizari Valerian
From Wikipedia, the free encyclopedia
Publius Licinius Valerianus (takriban 193/200 – 260/264) alikuwa Kaizari wa Dola la Roma kuanzia tarehe 22 Oktoba 253 hadi 260 alipotekwa na mfalme Shapur I wa Uajemi. Jambo hilo jipya lilitikisa dola lote.
Wakati alipoandaa vita yake dhidi ya Uajemi aliamuru sadaka kwa miungu ya Roma zitolewe pia na Wakristo. Aliposikia kwamba walikataa aliagiza kuua maaskofu; Wakristo wengine waliokuwa na cheo walipoteza cheo na mali na kuuzwa kama watumwa wakikataa sadaka hiyo[1]. Alitawala pamoja na mwana wake, Kaizari Galienus. Baada ya kifo cha baba yake, Galienus alisimamisha dhuluma dhidi ya Wakristo. Alimfuata Aemilianus.