Genoveva Torres Morales
From Wikipedia, the free encyclopedia
Genoveva Torres Morales (Almenara, 3 Januari 1870 - Zaragoza, 5 Januari 1956) alikuwa mtawa wa Kanisa Katoliki nchini Hispania ambaye, baada ya kupitia majaribu na maradhi mengi tangu utotoni, alianzisha shirika lake lijulikanalo kama Mabinti wa Moyo Mtakatifu wa Yesu na Malaika watakatifu. Alitaka shirika hilo jipya lizingatie utunzaji wa wanawake wote[1]. Wakati wa maisha yake na baada ya kifo chake, alitajwa kama "Malaika wa Upweke". [2]
Papa Yohane Paulo II alimtangaza mwenye heri mnamo 1995 na mtakatifu mnamo 2003. [3]