Filipo II wa Hispania
From Wikipedia, the free encyclopedia
Filipo II wa Hispania (kwa Kihispania Felipe II (el Prudente) (yaani Mwenye busara); 21 Mei 1527 – 13 Septemba 1598), alikuwa mfalme wa Hispania (1556–1598), Ureno (1581–1598), Napoli na Sicily (kuanzia 1554), na mume wa malkia Maria I wa Uingereza (1554–1558).[1] Alikuwa pia mtawala wa Milano[2] na kuanzia mwaka 1555 wa wilaya kumi na saba za Netherlands.
Dola lake lilienea katika mabara yote yaliyojulikana na Wazungu, na mpaka leo nchi ya Ufilipino inaitwa kwa jina lake (Visiwa vya Filipo). Chini yake, Hispania ilifikia kilele cha ustawi wake.