Domofupi
Ndege wadogo wa familia Paridae / From Wikipedia, the free encyclopedia
Domofupi ni ndege wa familia Paridae. Hawa ni ndege wadogo wenye domo fupi na mkia mfupi; spishi kadhaa zina kishungi. Rangi zao si kali sana: kwa kawaida nyeusi, nyeupe, kijivu na/au kahawia, pengine buluu, njano na nyekundu. Wanatokea Afrika, Asia, Ulaya na Amerika ya Kaskazini katika maeneo yenye miti. Hula wadudu na pia mbegu na makokwa. Hulijenga tago lao ndani ya tundu mtini. Jike huyataga mayai 3-19 yenye madoa.
Maelezo zaidi Uainishaji wa kisayansi, Ngazi za chini ...
Domofupi | ||||||||||||||
---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
Domofupi tumbo-jeupe | ||||||||||||||
Uainishaji wa kisayansi | ||||||||||||||
| ||||||||||||||
Ngazi za chini | ||||||||||||||
Jenasi 14:
| ||||||||||||||
Funga