Dominiko wa Silos
From Wikipedia, the free encyclopedia
Dominiko wa Silos, O.S.B. (Rioja, Hispania, 1000 - Silos, 20 Desemba 1073) alikuwa mkaapweke aliyefufua monasteri ya Silos nchini Hispania akawa abati wake. Alijitahidi kueneza urekebisho wa umonaki wa Kibenedikto lakini pia kukomboa Wakristo waliotekwa na Waislamu kama watumwa[1].
Tangu kale anaheshimiwa na Kanisa Katoliki kama mtakatifu.
Sikukuu yake inaadhimishwa kila tarehe 20 Desemba[2].