Benedikto Yosefu Labre
From Wikipedia, the free encyclopedia
Benedikto Yosefu Labre (kwa Kifaransa Benoît-Joseph Labré; Amettes, Boulogne-sur-Mer, Ufaransa, 25 Machi 1748 - Roma, Italia, 16 Aprili 1783) alikuwa Mkristo ambaye tangu ujanani alitamani sana maisha ya toba kali.
Kwa ajili hiyo aliiishi miaka mingi bila makao maalumu, akihiji kwa tabu nyingi makanisa mbalimbali akiwa amevaa nguo zilizochakaa na akila alichopewa tu, akitoa mfano bora wa ibada, hasa kwa kuabudu ekaristi.
Hatimaye alihamia Roma alipoishi katika sala na ufukara mkubwa sana.
Alitangazwa na Papa Pius IX kuwa mwenye heri tarehe 20 Mei 1859, halafu Papa Leo XIII akamtangaza mtakatifu tarehe 8 Desemba 1881.