Benedikto Menni
From Wikipedia, the free encyclopedia
Benedikto Menni, O.H. (Milano, Italia, 11 Machi 1841 - Dinan, Ufaransa, 24 Aprili 1914) alikuwa padri wa shirika la kihospitali la Mt. Yohane wa Mungu nchini Italia halafu Hispania, alipoanzisha shirika la Masista Wauguzi wa Moyo wa Yesu kwa ajili ya kuhudumia wahitaji wa kila aina[1][2][3][4].
Papa Yohane Paulo II alimtangaza kwanza mwenye heri tarehe 23 Juni 1985, halafu mtakatifu tarehe 21 Novemba 1999.