Augustino Roscelli
From Wikipedia, the free encyclopedia
Augustino Roscelli (Bargone, Casarza Ligure, 27 Julai 1818 – Genova, Liguria, 7 Mei 1902) alikuwa padri wa Kanisa Katoliki kutoka Italia Kaskazini[1].
Alianzisha shirika la kitawa la Masista wa Imakulata limsaidie kukabili matatizo ya jamii hasa upande wa malezi ya watoto na wanawake[2].
Alitangazwa na Papa Yohane Paulo II kwanza mwenye heri tarehe 7 Mei 1995, halafu mtakatifu tarehe 10 Juni 2001[3].