Yosefu wa Kopertino
From Wikipedia, the free encyclopedia
Yosefu wa Kopertino (Copertino 17 Juni 1603 – Osimo 18 Septemba 1663) alikuwa padri wa utawa wa Ndugu Wadogo Wakonventuali.
Mtu wa sala hasa, alijaliwa karama za pekee, hasa ile ya kuelea hewani kwa muda mrefu wakati wa kutoka nje ya nafsi.
Alitangazwa na Papa Benedikto XIV kuwa mwenye heri tarehe 24 Februari 1753, halafu Papa Klement XIII alimtangaza mtakatifu tarehe 16 Julai 1767.