Yosefu Moscati
From Wikipedia, the free encyclopedia
Yosefu Moscati (kwa Kiitalia: Giuseppe Moscati; Benevento, 25 Julai 1880 – Napoli, 12 Aprili 1927) alikuwa daktari na mwanabiolojia wa Italia Kusini[1].
Pamoja na kutibu wagonjwa bila kujibakiza, kwa huruma kubwa na hata bure, alikuwa anashughulikia roho zao pia, na pengine aliwaponya kimuujiza; pia alikuwa mtafiti wa biokemia na kufundisha chuo kikuu[2][3].
Alitangazwa mwenye heri na Papa Paulo VI tarehe 16 Novemba 1975, halafu mtakatifu na Papa Yohane Paulo II tarehe 25 Oktoba 1987.