Yohane wa Fiesole
From Wikipedia, the free encyclopedia
Yohane wa Fiesole, O.P. au Beato Angelico (yaani, kwa Kiitalia: "Mwenye heri wa Kimalaika"[2]; jina la awali: Guido di Pietro; Vicchio, Firenze, 1395 hivi[3] ā Roma, 18 Februari 1455) alikuwa mtawa padri maarufu kama mmojawapo wa wachoraji wa kwanza wa Renaissance nchini Italia. Mtaalamu Giorgio Vasari katika kitabu chake Maisha ya Wasanii aliandika kwamba alikuwa na "kipaji adimu na kamili".[4]
Tarehe 3 Oktoba 1982 Papa Yohane Paulo II alimtangaza rasmi kuwa mwenye heri,[5] kutokana na utakatifu wa maisha yake, si tu kwa kipaji chake cha kutoka mbinguni.[6]. Vasari huyohuyo aliandika kwamba "haiwezekani kumsifu mno baba huyo mtakatifu, aliyekuwa mnyenyekevu na mtaratibu hivi katika yale yote aliyoyafanya na aliyoyasema, na ambaye picha zake zilichorwa kwa unyofu na ibada kubwa hivi."[4]