Yohane wa Brebeuf
From Wikipedia, the free encyclopedia
Yohane wa Brebeuf, S.J. (Condé-sur-Vire, Normandy, Ufaransa 25 Machi 1593 – karibu na Midland, Ontario, Kanada, 16 Machi 1649) alikuwa padri wa Wajesuiti mmisionari kwa Wahuroni wa Amerika Kaskazini tangu mwaka 1625 (isipokuwa 1629-1633)[1].
Alikamatwa pamoja na Waindio hao, akateswa akauawa na Wairoki, kabila lingine la Waindio.
Alitangazwa na Papa Pius XI kuwa mwenye heri tarehe 21 Juni 1925, na kuwa mtakatifu tarehe 29 Juni 1930[2].
Sikukuu ya kundi lake la wafiadini huadhimishwa tarehe 19 Oktoba, lakini ya kwake mwenyewe huadhimishwa tarehe ya kifodini chake[3].