Yohane Maria Vianney
From Wikipedia, the free encyclopedia
Yohane Baptista Maria Vianney (Dardilly, 8 Mei 1786 – Ars-sur-Formans, 4 Agosti 1859), alikuwa padri mwanajimbo wa Kanisa Katoliki kutoka Ufaransa; kwa miaka zaidi ya 40 alifanya kwa namna ya ajabu kazi ya uchungaji kama paroko wa kijiji cha Ars, karibu na Belley, kwa kuhubiri mara nyingi, kusali na kufanya malipizi, huku sifa zake zikivutia watu kutoka nchi za nje ya Ulaya pia.
Kila siku katika katekesi aliyotoa kwa watoto na kwa watu wazima, katika upatanisho aliyowapatia walitobu na katika matendo yaliyojaa upendo wenye ari aliokuwa anauchota katika chemchemi ya ekaristi, alisonga mbele kiasi cha kueneza kila mahali mashauri yake na kusogeza kwa busara wengi kwa Mungu[1].
Alitangazwa na Papa Pius X kuwa mwenye heri tarehe 8 Januari 1905, halafu Papa Pius XI akamtangaza mtakatifu mwaka 1925 na msimamizi wa maparoko mwaka 1929.