Yohane Berchmans
From Wikipedia, the free encyclopedia
Yohane Berchmans (Diest, leo nchini Uholanzi, 13 Machi 1599 – Roma, Italia, 13 Agosti 1621) alikuwa mtawa katika shirika la Wajesuiti aliyefuata kikamilifu mfano wa Aloysius Gonzaga.
Mpendwa wa wote kwa unyofu wa moyo wake wa ibada, upendo halisi na uchangamfu wa kudumu, baada ya ugonjwa wa muda mfupi, kijana huyo alikabili kifo kwa utulivu [1].
Tarehe 28 Mei 1865 alitangazwa na Papa Pius IX kuwa mwenye heri, halafu tarehe 15 Januari 1888 akatangazwa na Papa Leo XIII kuwa mtakatifu.