Yesu kuzaliwa na Bikira
From Wikipedia, the free encyclopedia
Yesu kuzaliwa na Bikira ni fundisho la imani linalosema kuwa Yesu Kristo alitungwa tumboni mwa mama yake, Bikira Maria, kwa uwezo wa Mungu (Roho Mtakatifu) tu, na kuwa Maria alipomzaa alikuwa bado bikira.
Katika Biblia ya Kikristo fundisho hilo linapatikana katika Injili mbili zilizo tofauti hata kwa vyanzo katika uzazi na utoto wa Yesu: Math 1:18-25[1] na Lk 1:26-38[2].
Mathayo anathibitisha hilo kwa kutaja utabiri wa maneno ya Isa 7:14 katika tafsiri ya Kigiriki ya Septuaginta: "Tazama bikira atachukua mimba, naye atazaa mwana, nao watamwita jina lake Emmanuel, yaani Mungu pamoja nasi".[3] [4]
Fundisho hilo linashikiliwa na madhehebu karibu yote ya Ukristo, hasa Wakatoliki, Waorthodoksi na Waorthodoksi wa Mashariki.
Hata Waislamu wanakubali fundisho hilo kutokana na Kurani, hasa sura 3 (Al Imran) na 19 (Maryam (sura)).[5]