Wuhan
From Wikipedia, the free encyclopedia
Wuhan (kwa Kichina: 武汉) ni mji wa China. Ndio mji mkuu wa jimbo la Hubei.
Jiji la Wuhan | |
Mahali pa Wuhan katika China |
|
Majiranukta: 29°58′20″N 113°53′29″E | |
Nchi | China |
---|---|
Jimbo | Hubei |
Idadi ya wakazi | |
- Wakazi kwa ujumla | 9,760,000 (2,007) |
Tovuti: http://www.wuhan.gov.cn/ |
Kwa mujibu wa sensa iliyofanyika mnamo mwaka wa 2007, kuna wakazi wapatao milioni 9.8 wanaoishi katika mji huu[1]. Hivyo si mji mkubwa zaidi katika Hubei pekee, bali ni jiji kubwa zaidi katika China ya Kati.
Ni mji wenye tasnia nyingi, kuanzia makampuni yanayozalisha motokaa hadi makampuni ya teknolojia mpya kama kompyuta, pamoja na taasisi za utafiti wa kisayansi zaidi ya 300 [2].
Mwaka 2020 jina la Wuhan lilitajwa kote duniani kutokana na uenezi wa virusi hatari vya corona ambao ulisababisha vifo vya watu zaidi ya elfu moja pamoja na hofu ya epidemiki[3]. Jiji lote liliwekwa na serikali kuu katika hali ya karantini. Kabla ya tangazo hilo watu milioni 5 waliondoka mjini[4].