Tegla Loroupe
Mkimbiaji wa mbio ndefu na mwanaharakati wa usalama, elimu, na haki za wanawake / From Wikipedia, the free encyclopedia
Tegla Loroupe ni mwanariadha na mwanaharakati wa usalama, elimu, na haki za wanawake wa Kenya.
Loroupe alikuwa mwanamke Mwafrika wa kwanza kushinda Marathoni ya jiji la New York katika mwaka 1994 na aliweka rekodi ya ulimwengu ya marathoni.[1] Tegla Loroupe aliweka rekodi ya ulimwengu ya marathoni kutoka 19 Aprili 1998 hadi 30 Septemba 2001. Yeye bado ana rekodi ya ulimwengu kwa mashindano ya kilometa 25 na 30. Yeye alishinda shindano katika miji ya London, Boston, Rotterdam, Hong Kong, Berlin, Rome na miji mwingine.[2] Katika 2003, Loroupe aliunda taasisi ya fedha ya kuchangia amani na usalama ambayo inaitwa Tegla Loroupe Peace Foundation Archived 24 Julai 2019 at the Wayback Machine.. Kisha katika 2006, yeye aliunda mbio za Amani na Usalama za kilometa 10. Aidha, Loroupe alianzisha timu ya wakimbizi katika Olimpiki ya 2016.[3]