Stanislaus mfiadini
From Wikipedia, the free encyclopedia
Stanislaus mfiadini (kwa Kipolandi:Stanisław Szczepanowski; 26 Julai 1030 – 11 Aprili 1079) alikuwa askofu wa Kraków[1] kuanzia mwaka 1072 hadi kifodini chake [2].
Kati ya maonevu ya wakati wake, alitetea kwa nguvu zake zote ustaarabu na tunu za Kikristo na kuongoza jimbo lake kama mchungaji mwema akisaidia maskini na kutembelea kila mwaka waklero wake.
Anajulikana hasa kwa kuuawa wakati wa kuadhimisha ibada na mfalme wa Polandi Bolesław II ambaye hakupenda makemeo yake makali.
Kwa sababu hiyo Stanislaus alitangazwa mtakatifu mfiadini na Papa Inosenti IV tarehe 17 Septemba 1253.
Sikukuu yake huadhimishwa na Kanisa Katoliki kote duniani tarehe ya kifodini chake[3], lakini pia tarehe 7 Mei na 8 Mei, hasa nchini mwake.